12 Jul 2015

SALASALA VISION GROUP WAKABIDHIWA HATI ZA HEKARI 250 HUKO FUKAYOSI BAGAMOYO PIA YAZINDUA TOVUTI.

Afisa Mtendaji Mkuu EAG Group Iman Kajula Wa Pili (kushoto) akipokea hati ya Kimila ya eneo walillonunua bagamoyo kwajili ya Jumuiya hiyo.
Jumuiya iliyoasisiwa na wakazi wa Kilima hewa Salasala jijini Dar es salaam likiwa na malengo ya kijamii na kiuchumi. Tangu kuasisisiwa SVG imetekeleza miradi Mingi kwenye eneo la Salasala ikiwemo kupanda miti zaidi ya 5,000, kutengeneza barabara, kutengeneza viwanja vya michezo na kulinda maeneo ya wazi, Ulinzi, kutengeneza gari la polisi na misaada ya miradi mbalimbali endelevu ikiwamo kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa Salasala
 
SVG haikuishia hapo, imeamua kwa dhati kuchochea maendeleo ya Wanachama wake. Mradi mkubwa uliotekelezwa ni pamoja na kununua hekari 250 huko Fukayosi Bagamoyo. Baada ya ununuzi huu mchakato wakupata hati ulifanywa na kufanikiwa kupata hati za kimila na kukabidhiwa kwa wanachama wa SVG ili kuanza kuendeleza maeneno hayo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Aridhi wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Kibona aliipongeza SVG kwa kuwa kikundi kilicho makini na kutumia dhima ya umoja ni nguvu, alisema hati za kimila zina faida nyingi sana ikiwamo kutokuwa na kipindi cha ukomo ikilinganishwa na hati za kawaida.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SVG Yahaya Banka alisema ‘’ SVG inalenga kuendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa wanachama wake na familia zao. Tunaamini kwa kutumia nguvu ya umoja tunaweza kuleta maendeleo makubwa  katika eneo letu tunaloishi pia kwa familia za wanachama’’

MAANDAMANO YA AMANI YA WADAU WA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa nchi zilizoendelea ndio zinaongoza katika uharibifu wa mazingira kwa utumiaji wa Nuklia ,pamoja na uchimbaji wa Chuma hivyo zinawajibu kuwekeza katika mabadiliko tabia nchi kutokana na kuchangia hali hiyo .

Hayo ameyasema leo Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga wakati wa matembezi ya amani ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi yaliyofanyika  viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yamezidi kukua kwa kasi kutokana na uharibuifu wa mzingira unaofanywa na binadamu kwa shughuli za kila siku  huku jitihada za kukabili mabadiliko hayo zikichukua asilimia ndogo.

Mwanga amesema malengo 17 ya maendeleo endelevu ya tabia ya nchi  ya mwaka 2015 -2030  kunahitaji viongozi kushughulikia katika vyanzo mbalimbali vya fedha katika kuweza kufikia malengo na  kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara ya ukame,njaa, vifo pamoja na mafuriko.

Aidha amesema kuna mikutano mbalimbali inakuja hivyo ni kila mtu kwa nafasi yake ashiriki katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi iweze kuwa na uchumi imara.

 Wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegeme wakihamasisha urtunzaji wa mazingira katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee ya jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango mbalimbali yenye jumbe tofautitofauti ili kuhamasisha yamii kuachana na uchafuzi wa mazingira ili kuokoa maisha ya watanzania kutokana na kuwa na majamba mbalimbali yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia  ya nchi, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee wakiimba wimbo unaohamasisha utunzaji wa mazingira ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira kwa njia mbalimbali, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga akizungumza na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia  ya nchi mara baada ya kuhitimisha maandamano ya amani yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja ya wadau mbalimbali wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa na mabango ambayo yanahamasisha utunzaji wa mazingira pamoja na ujumbe wa kuokoa maisha ya jamii kwa kutunza mazingira, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

6 Jul 2015

2 Jul 2015

RAISI KIKWETE NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA WAZINDUA KIWANDA ZA KUDHIBITI MALARIA PWANI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo. Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi kabla uzinduzi wa kiwanda cha kudhibiti malaria Mkoani Pwani leo.

1 Jul 2015

Tazama Majina ya wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano, 2015/ 2016

OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.

Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.

  
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa nafursa ya mabadiliko yoyote ya shule. 

  
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho yakuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu,


MAELEKEZO: Matokeo yanatoka kwa kituo kizima ulichofanyia mtihani.

Jinsi  Ya  Kupata kituo  chako: 
Kwenye kisanduku anza kuandika jina la kituo ulichofanyia mtihani na usubiri, jina lililokamilika la kituo litajimalizia lenyewe ikiwemo namba ya kituo. 

Mfano: Iyunga, Halafu  Subiri  kidogo  ili  ijimalizie  yenyewe 

Ukishachagua utabofya neno 'retrive' na utapata majina ya shule yako yote uliyotoka. 

<< BOFYA  HAPA  KUONA  MAJINA>>